Mgogoro kati ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na klabu ya Yanga umefikia kikomo baada ya Serikali kuzikutanisha pande zote mbili na kila mmoja kutoa dukuduku lake.

Kikao hicho kimeitishwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuongozwa na katibu mkuu wake, Dk Hassan Abbas lengo likiwa kumaliza tofauti juu ya pande hizo mbili katika masuala mbalimbali ambayo yalikuwa hayaendi sawa na kuleta sintofahamu ambayo ilikuwa inaharibu taswira ya mpira nchini.

Katibu Mkuu wa Yanga, Mfikirwa amekiri kikao hicho kufanyika chini ya usimamizi wa Serikali na pande zote kufikia muafaka kwa faida ya soka la Tanzania.

“Nashukuru Serikali imetimiza ahadi yake ya kutukutanisha na uongozi wa TFF, na kueleza yale malalamiko yetu na pia nafurahi kuona muafaka umefikiwa kwa maslahi mapana ya mpira wa Tanzania, “amesema Mfikirwa.


Amuua mama mkwe alipojaribu kumsuluhisha na mkewe
Kisa Simba Queens, meneja asusa