Baada ya kuonekana lulu katika mchezo wa ligi wa mwishoni mwa juma lililopita kwa kufunga mabao mawili dhidi ya Crystal Palace, akitokea kwenye msukosuko wa kutoelewana na Pep Guardiola, kiungo kutoka nchini Ivory Coast Yaya Toure ameahidiwa makubwa huko Etihad Stadium.

Guardiola ambaye alichukizwa na kauli zilizowahi kutolewa na wakala wa kiungo huyo aitwae Diomitri Seluk, amesema alifurahishwa na uwezo wa Yaya katika mchezo dhidi ya Crystal Palace na anaamini mambo yatakaa sawa wakati wowote kuanzia mwaka 2017.

Guardiola amesema atalazimika kumrejesha Yaya katika kikosi cha Man city kinachoshiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya wakati wa majira ya baridi, kutokana na ujasiri wa upambanaji aliouonyesha.

Waandishi wa habari walimuhoji meneja huyo kutoka nchini Hispania, kwa kumuuliza kama anajutia maamuzi ya kumuweka nje kwa kipindi kirefu kiungo Yaya Toure mwenye umri wa miaka 33 alijibu: “Hapana. Akaulizwa tena kama atamsajili katika kikosi cha ligi ya mabingwa barani Ulaya wakati wa majira ya baridi akajibu, Ndio.”

“Nipo hapa kufanya maamuzi. Na labda nilifanya makosa, lakini ninalazimika kufanya maamuzi na ninaheshimu mawazo ya watu wengine hata wale ambao hawakubaliani na mimi.

“Sikubaliani na kilichotokea. Niliwahi kuzungumza mwezi uliopita, nimekua na Yaya kwa kipindi kirefu tangu tukiwa FC Barcelona, Ninamfahamu vizuri sana.

“Hivyo ninajua ni vipi alivyo. Kwa upande wa uchezaji wake sina tatizo — na kama kuna tatizo lingine siwezi kuingia kwa kina lakini ninazungumzia uchezaji wake ambao una umahiri mkubwa.

Yaya Toure alikua nje ya kikosi cha Man city kwa zaidi ya miezi mitatu kufuatia mikwaruzano iliyotokea baina ya wakala wake (Dimitri Seluk) na Pep Guardiola na aliahidiwa kurejea tena kucheza soka, mpaka waombe radhi kwa makosa yaliyojitokeza.

Ridhiwani Kikwete: Kuna Tatizo Yanga
Jose Mourinho Arudisha Majibu Kwa Michael Carrick