Mabingwa wa Soka Tanzania Bara (Young Africans) na Mabingwa wa Uganda (Vipers SC) watasherehesha kilele cha wiki ya Mwananchi, Jumamosi Agosti 06, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Mchongo huo umefahamika leo Jumatatu (Agosti Mosi), baada ya Uongozi wa Young Africans kuanika hadharani Mipango na Mikakati kuelekea Kilele cha Wiki ya Wananchi, katika Mkutano na Waandishi wa Habari, uliofanyika jijini Dar es salaam.

Huenda mchezo huo ukawawezesha Mashabiki wa Soka la Bongo kumshuhudia Mshambuliaji hatari kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati Cesar Lobi Manzoki anaewindwa na Simba SC huku dili hilo likiwa bado lina vuta nikuvute.

Hata hivyo inadaiwa kuwa Uongozi wa Simba SC upo katika harakati za kuhakikisha Mshambuliaji huyo anakuwa sehemu ya wachezaji watakaotambulishwa kwenye Tamasha ya Simba Day, ambalo litafanyika Jumatatu (Agosti 08), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Mwaka 2021 Young Africans iliialika Zanaco FC kutoka nchini Zambia katika sherehe za Wili ya Mwananchi, na mchezo huo ulimalizika kwa wenyeji kuambulia kisago cha 2-1.

Wazuia msafara wa Waziri kumpa kero ya maji
Simba SC, M-Bet wataja thamani ya udhamini mpya