Kumekuwa na mpango wa ujanja kutaka kuwakutanisha wasemaji wawili wa Yanga na Simba na kutaka kuwapatanisha.
Zoezi hilo lilikuwa lifanyike kimyakimya lakini taarifa zinaeleza limekwama baada ya wahusika kuushitukia mchezo huo.
Wahusika ni Msemaji Mkuu wa Yanga, Jerry Muro na yule wa Simba, Haji Manara ambao wanaonekana kutolewana.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT), imeelezwa juhudi hizo zilikuwa zimelenga kuwakutanisha wawili hao ili kumaliza figisu linaloendelea.
Lakini baadaye, wawili hao walishituka na Manara ndiye alionekana kukataa akisisitiza hakuwahi hata mara moja kumkashifu Muro.
“Manara alishitukia mchezo huo, akakataa kabisa kwa kuwa anasema kamwe hakuwahi kumkashifu Muro na tayari alifungua malalamiko yake TFF. Hivyo haoni sababu ya kukutana na Muro,” kilieleza chanzo.
“Tena Manara amesisitiza kwamba asingeona sababu ya kukutana na Muro ambaye amekuwa akionyesha kutojali uungwana kwa maneno mengi ya kashfa ambayo anaona si ya kiuweledi.”
Muro na Manara wamekuwa na upinzani mkubwa, ingawa Manara amekuwa akilalamika Muro kutoa maneno makali dhidi yake, dhidi ya viongozi wa juu wa Simba mambo anayoamini si ya kimichezo wala uugwana.
Chanzo: salehjembe

Sunderland Wamrejesha Emmanuel Eboue EPL
Chelsea Yatupwa Nje Barani Ulaya