Beki wa kati wa klabu bingwa nchini England, Chelsea, Kurt Happy Zouma amemkandamiza mchezaji mwenzake Diego Costa kwa kusema anapenda kudanganya anapokua uwanjani.

Zouma alizungumza jambo hilo, mara baada ya mchezo wa ligi mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Arsenal ambao walikubali kufungwa mabao mawili kwa sifuri.

Beki huyo aliyefunga bao la kwanza katika mchezo huo, alifanyiwa mahojiano na kituo cha televisheni cha beIN Sports, na kusema Costa hupenda kudanganya hata anapokua mazoezini na wakati mwingine huwaudhi wachezaji wengine kwa tabia hiyo.

Alisema ilikua ni vigumu kutambua tukio la mshambuliaji huyo kutoka nchini Hispania ambalo lilitokea kati yake na mabeki wa Arsenal Laurent Koscielny na Gabriel Paulista lakini mwishowe alijithibitishia katika picha za televisheni na kuabini Costa hakua mkweli wa jambo alilolifanya.

Hata hivyo beki huyo mwenye umri wa miaka 20, akaongeza kwamba hakushangazwa baada ya kujiridhisha tukio lililofanywa na Diego Costa, kwa kumuhadaa muamuzi huku akisisitiza wazi kwamba kila mmoja ndani ya Chelsea anamjua mtu huyo kwa udanganyifu.

Costa yupo kwenye hatari wa kuadhibiwa na chama cha soka nchini England FA, endapo itadhihirika alitenda makossa kwa makusudi ya kumuhadaa muamuzi Mike Dean ambaye aliishia kumuadhibu beki wa Arsenal Gabriel Paulista.

https://youtu.be/GyJT7MCXS_Q

Orodha Ya Wanamichezo Matajiri Duniani
Hatari Yawakabiri Watumiaji Wa Simu Za ‘Iphone’