Ikiwa ni miezi michache tu tangu wajitenge kwenye familia ya Kifalme, Prince Harry na mkewe Meghan Markle, wamelamba dili nono la kufanya Podcast katika mtandao wa Spotify.

Podcast hiyo mpya yenye thamani ya £30m ambazo sawa Bilioni 92 za Kitanzania, inatarajiwa kuanza kuruka baadaye mwezi huu, huku hii ikiwa ni dili lao la pili pamoja.

Mwezi Septemba mwaka huu iliripotiwa kwamba wamelamba mkataba mnono kutoka kutoka mtandao wa Netflix.

Netflix imeingia nao mkataba kwa ajili ya kutengeneza maudhui mbalimbali ikiwemo Makala, Filamu, na Vipindi, mkataba uliotajwa kuwa na thamani ya Dola Milioni 100 ambazo sawa na takriban Shilingi Bilioni 231 za Kitanzania.

Harry na mkeweMerghan walijitenga na familia ya kifalme mapema mwaka huu.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Desemba 19, 2020
Tanzania kuimarisha ushirikiano na nchi zilizo mwambao wa Bahari ya Hindi