Waziri wa Maji, Juma Aweso, amewatahadharisha wataalum wa Wizara ya Maji na wakandarasi wanaotekeleza miradi ya maji kutokuchezea miradi hiyo kwani watashughulikiwa ipasavyo, amesema kuwa wizara ya maji si wizara ya ukame.

Akizungumza na wananchi wa Kahama mbele ya Rais John  Magufuli, jana Januari 28, 2021, Aweso amesema  wizara yake itasimamia usiku na mchana kuhakikisha watanzania wanapata maji safi, salama na yenye kujitosheleza.

“Zipo kelele na malalamiko ambayo umetupa sisi wizara ya maji, sisi tumeyapokea na tumeyasikia, ninachotaka kuwaambia wataalamu wetu wa wizara ya maji na wakandarasi wanaotekeleza wizara ya maji ni kwamba vipo vya kuchezea, ukishiba chezea kitambi au kidevu si miradi ya maji; tutakushughulikia ipasavyo,”amesema Aweso

Aidha  amesema kuwa  wameweza kutekeleza miradi 48 ya maji  katika vijiji 69 huku miradi 24 bado ikiwa inaendelea,  na kuongeza kuwa  wamefanikiwa kuwakomboa akina mama wa Kahama kwa kutatua tatizo la maji.

Ndayiragije ajitetea Stars kutolewa 'CHAN'
Jeshi la polisi lafunguka kifo cha dereva wa lori