Serikali ya Tanazania, inatarajia kutumia ndege isiyo na rubani kwa ajili ya upimaji wa maeneo sambamba na kuweka mfumo unganishi katika masuala ya matumizi ardhi, huku ikiwa na mpango wa kujenga ofisi za Mikoa baada ya kupokea Shilingi 345 Bilioni kutoka World Bank.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula, wakati akifanya mahojiano maalum na kituo hiki na kusema hatua hiyo inatokana na changamoto zilizopo ikiwemo kukosekana kwa taarifa za wamiliki, kubebana na sehemu kubwa ya ardhi kutopimwa.

Amesema, katika kufanikisha zoezi hilo, Wizara inatarajia kuanza na maeneo yenye kiwango kikubwa cha ardhi ambayo yatapimwa na vifaa vya kusimikwa vyenye uwezo wa kupima kilomita za mraba mia moja kwa wakati mmoja, kitu ambacho kitasaidia kuleta ufanisi.

Maafisa Arhi nchini Tanzania wakiangalia ramani za makazi katika utendaji wa majukumu yao.

“Tunakwenda kuhakikisha kwamba katika suala la upimaji tunakuwa na zile points za kiwango kikubwa ambapo vifaa vitakavyosimikwa vitakuwa na uwezo wa kupima eneo kubwa kwa wakati mmoja na hii itasaidia sana,” amesema Waziri Mabula.

Kuhusu ndege zisizo na rubani, ambazo zinatarajia kupima ardhi, Waziri amesema zitarahisisha kazi nyingi kwa haraka kwa kuchukua picha za anga kabla ya kupima maeneo ardhini kitu ambacho kitatoa picha kamili kabla ya upimaji.

Amesema, hatua hiyo inatokana na sehemu kubwa ya ardhi nchini kutopimwa na kwamba eneo lililofanyiwa upimaji halizidi asilimia 25, hivyo mpango huo utasaidia kurahisisha mambo mengi kwa kuhama kutoka analojia kwenda digitali.

Wananchi wakiwa katika Kilimo, hizi ni moja kati ya matumizi ya ardhi Duniani.

“Sehemu kubwa ya ardhi hapa nchini haijapimwa na iliyopimwa haivuki hata asilimia 25 sasa kwakua tunahama kutoka anajia kwenda digitali ni wazi sasa kutakuwepo na urahisiswahi wa upimaji wa adrhi kwa kiwango kikubwa,” amefafanua Waziri.

Akizungumzia ujenzi wa ofisi za mikoa za ardhi, Dkt. Angelina amesema fedha hizo mbali na mambo mengine pia zitasaidia kuwezesha ujenzi huo kwa maeneo yote nchini ukitoa Mkoa wa Dar es Salaam ambao hauna hitaji hilo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mabula amesisitiza zoeli hilo kuendana na lile la anuani za makazi, ambalo litasaidia kurahisisha utoaji wa huduma kwa Wananchi ikiwemo kutambua idadi ya Wanzania wanaomiliki ardhi katika maeneo yao, namna ya kuwafikia na idadi yao kijumla.

Mfano wa upangaji wa miji katika ardhi iliyopimwa.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imepanga kufanya Sensa ya Watu na Makazi ifikapo Agosti 2022, kwa uratibu wa Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), ikishirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS).

Simba SC yajibu FUMBO la Nembo ya Mdhamini
Ivory Coast yaitaka Mali kuwaachilia wanajeshi wake