Maneno machafu waliyozoea kuyatamka wasanii wa Marekani kwenye nyimbo zao na wawapo jukwaani yamemgharimu 50 Cent alipokuwa akipiga show kubwa wikendi mbele ya watu 40,000, St. Kitts, Caribbea.

Rapa huyo ambaye awali alipewa muongozo wa ustaarabu wa kufanya tamasha kwenye eneo hilo akitakiwa kutotumia maneno machafu, alijikuta mikononi mwa polisi baada ya kupandwa na mizuka jukwaani na kutamka ‘mother f***k’ kama alivyozoea kujidai na lugha hizo akiwa Marekani.

Neno hilo halitakiwi kutamkwa hadharani katika eneo hilo na limekatazwa katika sheria na adhabu yake kuanishwa.

Kwa mujibu wa TMZ, Polisi walimstahi kwa muda rapa huyo hadi alipomaliza kufanya kazi yake jukwaani na alipoteremka walimkamata na kumfikisha kwenye kituo cha polisi akitarajiwa kufikishwa mahakamani leo.

Atalazima kusubiri maelekezo na uamuzi wa Mahakama akitarajiwa kulipa fidia kwa kufanya kosa hilo.

 

Lionel Messi Atangaza Kustaafu Soka
Rais ampongeza Dj Black Coffee kwa kuwapenya Diamond, Wizkid