Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, linawashikilia watuhumiwa 62 kwa makosa mbalimbali wakiwepo wahalifu walio kamatwa na vifaa vya mradi wa umeme katika Bwawa la mwalimu nyerere na nyara za Serikali.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, ACP. Protas Mutayoba amesema Jeshi hilo liliendesha operesheni katika mkoa huo na kufanikiwa kukamata mtungi wa gesi uliokuwa unakwenda katika mradi huo wa mwalimu Nyerere.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, ACP. Protas Mutayoba akionesha moja ya nyara za Serikali zilizokamatwa.

Amesema, Jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata watuhumiwa wa madawa ya kulevya, pikipiki zinazotumika katika uhalifu pamoja mtuhumiwa ambaye amekutwa na nyara za Serikali.

Aidha, Kamanda Mutayoba ameeleza kuwa Jeshi hilo liliendesha operesheni ya usalama Barabarani ambapo walikamata jumla ya makosa mbalimbali 8,035huku likitoa rai kwa wananchi kutoa taarifa za uhalifu na walifu ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

CCM yapitisha marekebisho katiba ya chama
Ajali ya Cruiser gari la Jeshi na pikipiki: Vilio vyatawala msibani