Kiungo wa Arsenal Aaron Ramsey amesema wapo tayari kupambana na kufikia lengo la kuzinyakua point tatu muhimu katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili, ambao utawakutanisha na mahasimu wao wakubwa wa kaskazini mwa jijini London Tottenham Hotspurs.

Ramsey amesema litakua jambo la kujivunia kufanya vizuri katika mchezo huo, kutokana na kikosi cha Arsenal msimu uliopita kufanya maajabu ya kumaliza juu ya Spurs kwenye msimamo wa ligi, baada ya kushinda mchezo wao wa mwisho.

“Kwa sasa tupo katika hali nzuri ya kujiamini kutokana na maandalizi yanayoendelea kufanywa na benchi letu la ufundi,” Alisema Ramsey alipoulizwa kuhusu matarajio ya mchezo dhidi ya Spurs.

“Ni miaka mingi tumekua tunafanya maajabu dhidi yao kwa kumaliza ligi tukiwa juu, lakini wakati mwingine hutokea tunafanya hivyo bila kuwafunga ama wanatufunga, ila naamini itapendeza zaidi kama tukifanikisha lengo kama hilo huku tukijivunia kuwashinda wapinzani wetu.

“Kwa kweli wamekua wapinzani wenye hadhi kubwa dhidi yetu, na kila tunapokutana mambo huwa magumu, lakini kwa mchezo wa mwishoni mwa juma hili sina shaka, tutafanya vizuri.

“Tunajua bado Spurs hawajapoteza mchezo tangu tulipoanza ligi mwezi Agosti, na huenda jambo hilo likawapa chachu ya kuongeza ushindani dhidi yetu, lakini naamini tupo vizuri na tutakuwa wa kwanza kuwafunga.”

Hata hivyo kikosi cha Arsenal, nacho kipo katika mlolongo mzuri wa kupata matokeo mazuri, kwani mpaka sasa wameshacheza michezo 15 ya michuano yote bila kufungwa, achilia mbali mpambano dhidi ya Liverpool ambao walibamizwa mabao manne kwa matatu.

Usajili Wa Kun Aguero Waisumbua Real Madrid
Video: Machinga watua Bungeni Dodoma, Serikali yatoa majibu