Mwanamuziki Adele ameahirisha onyesho lake kubwa lililokuwa lifanyike Caesars Palace Vegas kwa madai ya mlipuko mkubwa wa COVID kwa wafanyakazi wake, huku baadhi ya vyanzo vikisema kuwa sababu halisi ya onyesho hilo kuahirishwa ni kutokana na Adele kutofurahishwa na maandalizi ya onyesho hilo.

Kwa mujibu wa TMZ inaelezwa kuwa Adele hakufurahishwa na mpangilio mzima wa mfumo wa maandalizi ya tukio hilo ikiwamo, kwaya, mfumo wa sauti na vitu vingine kadhaa vinavyohusika na onyesho hilo jambo lililompelekea mwimbaji huyo kuchukua uamuzi wa kuahirisha onyesho hilo katika hatua za mwisho.

Minong’ono iliyoibuka baada ya uamuzi huo wa Adele, ni kwamba waandaaji wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii kwenye kila kipengele cha maandalizi ya onyesho hilo tangu Desemba 2021, hivyo kitendo cha kuahirishwa ghafla kimeibua sintofahamu miongoni mwa waandaji na mashabiki wa mwanamuziki huyo.

Imani ya wengi ni kuwa suala hilo limetokana na Adele kutoridhishwa na matokeo ya maandalizi na si kuhusu athari za COVID kwa baadhi ya watu kutoka katika timu yake.

Hassan Mwakinyo akanusha kuvuliwa Ubingwa
Rais Samia atoa maagizo kwa RC Makalla