Muimbaji nyota wa Pop, Adele ametoa takriban dola millioni 58 ambazo ni zaidi ya tsh Bilioni 133.7 kwa ajili ya kununua jumba la kifahari la muigizaji nyota wa Hollywood mkongwe Sylvester Stallone maarufu Rambo lililopo Beverly Hills.

Adele anaripotiwa kuwa mbioni kumiliki jumba hilo kubwa baada ya Rambo kupunguza bei kidogo kutokana na wateja kushindwa kumudu gharama za awali zilizokuwa zikifika hadi dola milioni 110 sawa na tsh Bilioni 253.6 za Kitanzania.

Jumba hilo linaingia kwenye jalada la mali anazomiliki Adele linalotajwa kukua kwa kasi, ambalo tayari  lina nyumba zenye thamani ya takriban dola million34.7 huko London na LA.

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 33, ambaye kwa sasa yuko kwenye mahusiano ya kimapenzi na wakala wa michezo Rich Paul, 40, anasemekana kuwa na thamani ya pauni milioni 140 kutokana na rekodi yake ya mauzo yenye kuendelea kukua kwa kasi.

Mtoto mchanga aokotwa ndani ya choo cha ndege
Polisi Afrika Kusini inamshikilia mtu mmoja anayehusishwa na Moto uliounguza Bunge.