Jeshi la polisi nchini Misri limemtia mbaroni admin wa ukurasa maarufu wa Facebook aliyeweka maoni yake kuhusu uchepukaji wa wanawake wenye ndoa.

Admin huyo aliyetajwa kwa jina la Taymour el-Sobky, ambaye pia hufanya kipindi maarufu cha Television nchini humo alieleza kuwa wanawake wengi walioolewa huchepuka, hususani walioolewa katika ndoa za mitala.

Maelezo yake yalirushwa kwenye kipindi chake Desemba kupitia kituo cha CBC lakini hayakuzua gumzo sana hadi yalipotua kwenye ukurasa wake wa facebook wenye wafuasi zaidi ya milioni moja.

“Siku hizi, ni kawaida kwa wanawake kuchepuka na kutafuta wanaume nje ya ndoa… wanawake wengi wanajihusisha na masuala ya uhusiano wa ziada hasa wakati wanaume wao wakiwa nje ya nchi,” ilisomeka sehemu ya maelezo yake.

Muendesha mashtaka wa serikali alifungua mashtaka dhidi ya el-Sobky akimtuhumu kuwadhalilisha wanawake na kuwashushia heshima.

Nchini Misri, ni kosa kubwa na aibu kubwa kwa mwanamke kuchepuka. Sheria kali huchukuliwa dhidi ya mwanamke anaebainika kufanya kosa hilo.

Jack Cliff, aliyefungwa China kwa dawa za kulevya aandika barua ya wazi, iko hapa
Museveni amuonya Mpinzani wake kutotumia mbinu hii iliyotumiwa na ‘Ukawa’