Mkazi wa Kitongoji cha Manyala, kijiji cha Nyambage wilayani Butiama, mkoa wa Mara, Katamala Jackson ( 29) amefariki dunia kwa kuzama kwenye bwawa baada ya kushindana na wenzake kuogelea ambapo mshindi angepatiwa fedha tasilimu TZS 4,000.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mratibu Msaidizi Augustino Magere amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo ameeleza kuwa marehemu alikiwa akicheza mpira na wenzake na ndipo wakaanza kushindana kuogelea kwenye bwawa.

”kwa bahati mbaya Katamala alipofika kwenye kina kirefu cha maji alikosa pumzi na kupelekea kufariki dunia. jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi tulifanikiwa kuuopoa mwili huo ambao ulikuwa umenasa kwenye tope katika bwawa hilo.” amesema Kamanda Magere.

Kamanda Magere amepiga marufuku wakazi wa kitongoji hicho kuogelea katika bwawa hilo na kuwataka viongozi wa serikali ya kijiji kusimamia maagizo ya serikali ili bwawa hilo litumike katika matumizi yaliyokusudiwa

Habari Picha: Waziri Mkuu atembelea soko la Mbauda
Chaneli rasmi ya mtandao wa YouTube ya Dar24 Media imerudi hewani