Waziri wa elimu ya juu nchini Afghanistan  Abdul Baqi Haqqani amesema wanawake wataruhusiwa kusoma lakini hawatasoma pamoja na wanaume.

Haqqan ameeleza hayo baada ya wanamgambo wa Taliban kupandisha bendera  katika Ikulu ya Rais na sera mpya, ikionesha ishara ya mwanzo wa utawala wao tangu walipochukua udhibiti Agosti 15.Pia ametangaza masomo ambayo yatakuwa yanafundishwa.

Wanawake na wasichana walipigwa marufuku kusoma shule na vyuo chini ya sheria ya Taliban kati ya mwaka 1996 na 2001.

Aidha Taliban wamesema hawatazuia wanawake kupata elimu au kuwa na ajira. Lakini tangu wamechukua taifa hilo Agosti 15, wamewataka wanawake wote isipokuwa wale wanaofanya kazi katika sekta ya afya kutofanya kazi mpaka hali ya kiusalama itakapoimarika.

Wanafunzi wasichana walikuwa hawapewi kipingamizi cha mavazi na vyuo vikuu vilikuwa na wanafunzi mchanganyiko wanaume kwa wanawake.Lakini Haqqani hajaonesha kusikitishwa na maamuzi hayo.

 “Hatuna tatizo katika kusitisha mfumo wa elimu ya mchanganyiko ,Watu wetu ni waislamu hivyo watakubali.”Amesema Haqqani

Baadhi wametoa mapendekezo yao kuwa sheria mpya zinawatenga wanawake katika kupata elimu kwa sababu vyuo havina rasilimali za kutosha kwa ajili ya kuwa na madarasa tofauti.

Haqqani amesisitiza kuwa kuna walimu wa kike wa kutosha na kama hawatatosha watatafuta mbadala.Wasichana na wavulana pia watatengwa katika shule za msingi na sekondari, kitu ambacho kilikuwa kimezoeleka Afghanistan kote.

Wanawake watatakiwa kuvaa hijabs, hata hivyo Haqqani hakufafanua kama itakuwa lazima kuwa hijabu za kufunika uso au la.

Serikali yachukua hatua mbalimbali kupambana na Covid-19
Sudan:Mafuriko yaua watu zaidi ya 70