Mwanaume mmoja wa Fresno, California nchini Marekani amehukumiwa kifungo cha miaka 1,503 jela kwa kosa la kumbaka mwanae mdogo wa kike, kifungo ambacho kinatajwa kuwa kirefu zaidi katika eneo la Fresno.

Mahakama ya Fresno ilimhukumu Rene Lopez (41) kifungo hicho Ijumaa iliyopita, baada ya kuthibitisha bila shaka yoyote kuwa alikuwa akimbaka mwanae wa kike kwa kipindi cha miaka minne, tangu Mei 2009 hadi Mei 2013 ambapo msichana huyo alipata ujasiri wa kutoroka na kutoa taarifa.

Waendesha mashtaka waliieleza Mahakama kuwa kwa mara ya kwanza msichana huyo alibakwa na rafiki wa baba yake lakini alipoenda kushtaki kwa baba yake (Lopez), alianza kumgeuza chombo chake cha starehe cha ngono.

Ilielezwa kuwa Lopez alikuwa akimbaka mwanae kati ya mara tatu na mara nne kila wiki kwa kipindi chote cha miaka minne.

Mahakama hiyo ya Juu ya Fresno ilimkuta Lopez na hatia ya makosa 186 ya unyanyasaji wa kingono yakiwemo makosa mengi ya ubakaji wa mtoto mdogo.

Akisoma adhabu dhidi ya Lopez, Jaji Edward Sarkisian Jr. Alisema, ”Lopez ni mtu hatari sana kwenye jamii.”

Kanye West awatishia nyau waandaaji wa tuzo za Grammy
Live kutoka Ikulu: Ziara ya Mfalme wa Morocco, Mohamed VI nchini Tanzania