Hospitali ya Aga Khan kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la Reconstructing Women International (RWI), na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wameendesha programu ya upasuaji wa kubadili na kuboresha maumbile ya wanawake na wasichana waliopata madhara mbalimbali ya viungo vya mwili kutokana na ajali, majanga ya moto na saratani.

Upasuaji huo, unaofanyika bure unafadhiliwa na programu ya ustawi wa wagonjwa ya hospitali ya Aga khan pamoja na wabia wa makampuni mbalimbali inahusisha Madaktari bingwa wa upasuaji kutoka Marekani, Canada na Swetzwerland.

Akizungumza na waandishi wa Habari hii leo jijini Dar es Salaam, Daktari Bingwa wa upasuaji kutoka Hospitali ya Aga Khan, Aidan Njau amesema tangu kuanzishwa kwa programu hii mnamo mwaka 2016 wamefanikiwa kutibu wanawake na wasichana wapatao 220 ambapo kwa mwaka huu pekee tayari wanawake 23 wamwshanufaika na programu hiyo.

Madaktari katika chumba cha upasuaji. Picha ya FSF IHCE

Aidha, amesema programu hiyo imekuwa na manufaa makubwa sio tu kwa wananchi pekee bali kwa madaktari na watoa huduma ambapo husaidia kubadilishana utaalamu na vifaa vya kisasa vinavyowezesha kufanya matibabu hayo kwa ufanisi na weledi zaidi

Kwa upande wake, Mkuu wa upasuaji wa kubadili na kuboresha maumbile kutoka Hospitali yaTaifa ya Muhimbili, Dkt. Edwin Mrema amesisitiza wadau wa sekta ya afya nchini kutoa elimu kwa jamii juu ya njia sahihi za kuzuia na kujikinga na majanga ya moto ambayo kwa kiasi kikubwa ndio yamepelekea athari kubwa katika viungo vya miili ya wagonjwa waliopokelewa.

Naye, Daktari wa upasuaji wa kuboresha maumbile ambaye pia ni kiongozi wa timu ya Reconstructing Women International(RWI), Andrea Pusic amesisitiza kuendeleza ushirikiano baina ya hospitali hizo kwa lengo la kuwapa madaktari wakaazi wa upasuaji mafunzo ya mbinu za upasuaji wa kubadili na kuboresha maumbile ili kusaidia kurejesha utendaji wa kimwili kwa wanawake na hatimaye kuchangia katika uzalishaji na kukuza uchumi wa taifa.

Mlipuko Shuleni wauwa Wanafunzi 10
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Decemba 2022