Mwanamke mmoja ameripotiwa kujiua yeye na mwanae kwa kujirusha kutoka ghorofa ya tisa akidaiwa kukasirishwa na mwonekano wa pua yake baada ya kufanya upasuaji ili aongeze mvuto!

Mwanamke huyo wa Urusi aliyetajwa kwa jina la Anna Ozhigova mwenye umri wa miaka 33, anadaiwa kueleza hasira zake kwenye mtandao wa Facebook akimtumia ujumbe rafiki yake kuwa tangu afanyiwe upasuaji pua yake ilikuwa kama ya nguruwe.

Alieleza kuwa muonekano huo wa pua yake ulisababisha aachane na mumewe aliyezaa naye mtoto huyo kwani kila alipokuwa akimuona aliigiza sauti ya mlio wa nguruwe. Alidai kitendo hicho kilimnyima raha na kujiona hafai.

Anna Ozhigova, mumewe na mtoto wao

Anna Ozhigova, mumewe na mtoto wao

Kamati maalum ya Upelelezi ya Urusi inayofanya kazi sawa na FBI ya Marekani, imeeleza kuwa ujumbe huo alioutuma kwa rafiki yake ulieleza kwa kina sababu ya kuchukua uamuzi huo wa kujiua.

Ozhigova alimueleza rafiki yake huyo kuwa anajuta kufanya upasuaji wa pua yake na kwamba alishawishiwa na mtu mmoja kuwa angeongeza mvuto, lakini tangu afanye upasuaji huo hawezi hata kutabasamu.

”Tabasamu langu limevurugika kwa sababu aliondoa misuli juu ya mdomo na akabadili kitu fulani,” mwanamke huyo alimuandikia rafiki yake. ”Mume wangu alikuwa akiniona anatoa mlio kama wa nguruwe,” aliongeza.

Uamuzi wa kujirusha na mwanae unadaiwa kuwa hakutaka mwanae achukuliwe na mtu yeyote hususan mume wake huyo.

Kabla ya kuruka kutoka ghorofani akiwa amemshikilia mwanae huyo aliandika, ”Nilitaka furaha, wema na amani kwa mwanangu Gleb. Lakini anakuwa katika hali ya hasira.”

Kamati ya Upelelezi ya nchi hiyo imeeleza kuwa inaendelea na uchunguzi  wa kina juu ya tukio hilo.

Tarehe Ya Kuanza Mtanange Wa Ligi Daraja La Pili Yawekwa Wazi
Ronaldinho Gaucho Arejea FC Barcelona