Joto la kuondoka kwa mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Olympique Lyonnais Alexandre Lacazette ambaye anawaniwa na klabu ya Arsenal ya jijini London – England, limeendelea kupanda kufuatia uongozi The Kids kupanga mikakati ya kumsaka mbadala wake.

Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Loic Remy, anatajwa kuwa katika harakati za kuwaniwa na viongozi wa Olympique Lyonnais ambao wanaamini atawafaa kuziba nafasi ya Lacazette endapo itatokea anaondoka katika kipindi hiki.

Gazeti la The Daily Mail limeripoti kuwa, uongozi wa Lyon unaamini huenda ukampata kwa urahisi Remy katika kipindi hiki tofauti na kwa mshambuliaji mwingine yoyote, kutokana na mipango ya meneja wa Chelsea Antonio Conte kutomuhitaji huko Stamford Bridge.

Alexandre Lacazette

Remy mwenye umri wa miaka 29, amekua hana nafasi katika kikosi cha kwanza tangu alipojiunga na Chelsea akitokea Newcastle Utd mwanzoni mwa msimu 2014-15, jambo ambalo limekua likimpa kikwazo cha kuendeleza makali yake kama alivyokua nchini kwao Ufaransa akiwa na klabu ya Olympique de Marseille.

Kitendo cha Lacazette cha kufunga mabao matatu katika mchezo wa ufunguzi wa ligi ya nchini Ufaransa (Ligue 1) mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya  Nancy, kimeongeza kasi kwa Arsenal kuhitaji huduma ya mshambuliaji huyo.

Video: Tofauti ya Hotel, Motel na Lodge
Drinkwater Awagomea Leicester City, Spurs Wachekelea