Chama cha Upinzani cha Kisoshalisti Nchini Algeria (FFS), kimetangaza kususia Uchaguzi wa Bunge uliopangwa kufanyika Juni 12 kikisema mazingira ya kufanyika Uchaguzi huo hayaridhishi.

Baraza la Taifa la Chama hicho limesema matayarisho kuelekea Uchaguzi huo siyo rafiki, na Uchaguzi wenyewe hautatoa suluhisho la mizozo inayokabili sekta mbalimbali Nchini Algeria.

Baada ya kutangaza kulivunja Bunge mwezi uliopita, Rais Abdelmadjid Tebboune alitoa amri ya kufanyika Uchaguzi wa Bunge.

Hata hivyo maelfu ya raia waliandamana kupinga Uchaguzi huo wakati wa vuguvugu la kudai demokrasia la Hirak likishika kasi.

Hospitali ya Taifa Muhimbili yatoa ufafanuzi kufuatia ujumbe wa Kigwangala
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Aprili 4, 2021