Mkali wa ‘Aje’, Ali Kiba jana aling’ara zaidi katika tuzo za EATV 2016 zinazoandaliwa na kituo cha runinga cha East Africa zilizotolewa katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye huku msema chochote akiwa mtangazaji wa zamani wa kituo hicho, Salama Jabir.

Kiba aliongoza orodha kwa kunyakua tuzo tatu katika vipengele vyote vitatu alivyokuwa akiwania. Tuzo ya kwanza ni Msanii Bora wa Kiume, Wimbo Bora wa Mwaka (Aje), na Video Bora ya Mwaka (Aje).

Akitoa neno la shukurani mara tatu, Mfalme Kiba alisitiza kuwa tuzo hizo ni za mashabiki wake waliomuwezesha na kwamba yeye anachukua tu kwa niaba yao.

Tuzo nyingine nzito ya heshima ilienda kwa DJ Bony Love, aliyekuwa mmiliki wa studio za Mawingu na mmoja kati ya waasisi wa muziki wa Bongo Flava.

bonny-love

Hii ni orodha kamili ya washindi:

  1. Mwanamuziki Bora wa Kiume – Ali Kiba.

 

  1. Wimbo Bora wa Mwaka – Aje wa Ali Kiba.

 

  1. Video Bora ya Mwaka – Aje ya Ali Kiba.

 

  1. Mwanamuziki Bora wa Kike – Lady Jay Dee.

 

  1. Tuzo ya Heshima inayotolewa kwa mtu/taasisi yenye mchango mkubwa katika sanaa ya Tanzania inakwenda kwa Dj Bonny Love.

 

  1. Tuzo ya Filamu Bora ya Mwaka – ‘Safari ya Gwalu’ ya Gabo Zigamba.

 

  1. Mwigizaji Bora wa Kiume – Salim Ahmed maarufu Gabo Zigamba.

 

  1. Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike- Chuchu Hans.

 

  1. Kundi Bora la Muziki – Navy Kenzo

 

  1. Mwanamuziki Bora Chipukizi – Mwanamuziki Man Fongo

 

Anthony Joshua amtwanga Molina, uso kwa uso na Mbabe Klitschko Aprili
Kona ya Penzi: Jinsi ya kumjibu mpenzi anapouliza ‘Unanipenda Kiasi Gani?’