Ali Kiba amepata nafasi ya kubadilishana mawazo na kujiachia na Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Raila Odinga katika jiji la Mombasa ambalo ni maarufu zaidi nchini humo kama jiji la ‘raha’.

Odinga ambaye pia ni Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha ODM amepost kwenye akaunti yake ya Facebook, picha inayomuonesha akiwa na Ali Kiba pamoja na Gavana wa jiji hilo, Hassan Joho.

“Enjoying a pleasant evening in Mombasa with Hassan Joho and Ali Kiba. I hope you are enjoying yours. RAO,” ameandika kwenye picha hiyo.

Raila Odinga anatarajiwa kuwa mgeni maalum kwenye tamasha kubwa la muziki litakalofanywa na Chris Brown jijini humo leo. Ali Kiba na Vanessa Mdee ni kati ya wasanii watakao-share jukwaa moja na Breezy kuwapa mashabiki ‘kile roho yao inapenda’.

Tamasha hilo la Chris Brown linatarajiwa kuwavuta wana Afrika Mashariki kuijaza Mombasa leo.

Bodi ya Mkopo yashusha rungu kwa walimu waliompiga mwanafunzi kikatili
China yajadili kumng’oa Kiongozi wa Korea Kaskazini na jeshi lake