Mzee wa miaka 60, anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Longisa baada ya mtoto wake wa kiume Charles Kiplangat Rotich (22), kumtupa kwenye shimo lenye kina cha futi 20 kufuatia mzozo wa ardhi katika kijiji cha Emitiot, KILICHOPO Kaunti ya Bomet nchini Kenya.

Mwathiriwa, Samuel Tanui, alikaa siku mbili ndani ya shimo hilo bila kujulikana na siku ya tatu alifanikiwa kutoa sauti kubwa baada ya kusikia sauti za baadhi ya watu wakipita karibu na eneo hilo na ndipo wakamuokoa ambapo alikimbizwa hospitali kwaajili ya matibu.

Hata hivyo, mshukiwa Charles, alikamatwa na Polisi na kufikishwa katika kituo cha Longisa baada ya kurejea nyumbani usiku akidhani babake amefariki.

Baadhi ya taarifa kutoka kwa majirani, zinasema kuwa kijana huyo, alifanya kitendo hicho baada ya baba yake kukataa kumruhusu kuuza kipande cha ardhi ya familia.

Mgogoro wa ardhi wasabaisha mifugo kufa, mazao kuharibika
Baraza la Habari lachukua hatua udhibiti Wanahabari feki