Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 42 amemuua mkewe na baadaye kujiua nyumbani kwao, Kaunti ya Kiambu nchini Kenya.

Kwa mujibu wa ripoti za jeshi la polisi, Jonathan Gachunga alikuwa anamiliki silaha kihalali kwa mujibu wa sheria, alimuua mkewe kwa kumpiga risasi kichwani na baadaye akajipiga risasi kichwani wakiwa chumbani.

Miili ya wawili hao ilikutwa ndani ya chumba chao cha kulala Jumanne jioni, baada ya rafiki wa Gachung kuripoti katika kituo cha polisi kuwa rafiki yake hapokei simu kwa muda mrefu hali inayompa wasiwasi.

“Rafiki huyo pamoja na maafisa wa polisi walienda katika nyumba ya wawili hao ambapo chumba cha kulala kilikuwa kimefungwa. Mlango ulibomolewa na miili ya Gachunga na mkewe Phelomena Njeri ilikutwa,” inaeleza ripoti ya polisi.

Miili ya marehemu ilipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kenyatta kwa ajili ya kuihifadhi katika chumba cha kuhifadhi miili ya marehemu, ikisubiri kufanyiwa uchunguzi.

Chanzo cha mauaji hayo hakikufahamika kwa haraka.

Kesi ya Mbowe yahairishwa kisa mtandao
Mawaziri wa Afya Tanzania,Kenya kukutana leo