Mtoto wa miaka minne amenajisiwa na kuvunjwa shingo kisha kutupwa kandokando ya njia ya watembea kwa miguu karibu na mfereji wa maji umbali wa mita 50 kutoka nyumbani kwao jijini Arusha.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Yusuf Ilembo, tukio hilo la kunajisiwa kwa mtoto huyo wa kike lilitokea Juni 20, mwaka huu saa 3.30 usiku kwenye makaburi ya baniani Kata ya Unga Limited.
Kaimu Kamanda wa Polisi Ilembo Arusha jana alisema kuwa mtoto huyo ambaye kwa sasa ni marehemu alikuwa akicheza na wenzake nje kidogo ya nyumbani kwao na ilipofika saa 12 jioni kwa mujibu wa marafiki zake (majina yamehifadhiwa) wanasema alifika mtu mmoja mwanamume mrefu.
Kwa mujibu wa watoto hao, mwanamume huyo alikuwa amevaa suruali na kumwambia mtoto huyo amfuate akamnunulie pipi na hapo ndipo alipomfuata huyo mwanamume huyo na hakurudi tena mpaka alipokutwa akiwa ameshauawa kikatili.
Wananchi wanaombwa kutoa taarifa pindi waonapo dalili za uovu katika maeneo yao kwa viongozi au kituo chochote cha polisi kilichopo karibu.
Chidi Benzi Afunguka Chanzo cha Kutumia Madawa
Mipango Ya Jose Mourinho Yawavuruga Mashabiki Wa Soka