Wakala wa mshambuliaji kutoka nchini Nigeria, Umar Sadiq amefichua siri ya kufuatiliwa kwa mchezaji huyo na wasaka vipaji wa klabu ya Arsenal inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini England.

Mohammed Lawalb, wakala wa mshambuliaji huyo anayecheza kwa mkopo katika klabu ya AS Roma akitokea kwenye klabu ya Spezia Calcio inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Italia (Sirie B), amesema kumekua na mwenendo mzuri kwa mchezaji wake kufuatiliwa na watu wa Arsenal.

Taarifa za awali zinadai kwamba, The Gunners wapo tayari kumsajili Umar mwenye umri wa miaka 19, mwishoni mwa msimu huu kwa ada ya uhamisho wa paund million 13.

Katika msimu huu, Umar ameshafanikiwa kufunga mabao matano katika michezo tisa ya michuano ya UEFA kwa vijana, huku akifunga magoli mengine mawili katika mshikemshike wa ligi ya nchini Italia Serie A, ambayo ameitumikia mara sita.

Mohammed Lawalb, amesema kwa sasa mchezaji wake yupo katika hatua nzuri za kutaka kuelekea nchini England, kama mambo yatakwenda sawa, lakini akasisitiza jambo hilo litategemea baraka za viongozi wa klabu ya Spezia Calcio.

Hata hivyo amedai kwamba, Umar anafuatiliwa na watu wa klabu ya Borrussia Dortmund, hivyo huenda ushindani wa kusajiliwa kwake ukawa mkubwa itakapofika mwishoni mwa msimu huu.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger pia ameripotiwa kuwafuatilia wachezaji wengine wawili kutoka nchini Nigeria, Kelechi Nwakali na Samuel Chukwueze ambao kwa sasa wana umri wa miaka 19.

Mbeya City Kujiuliza Kwa Africans Sports Leo
Costa Kutumikia Adhabu Kwa Mchezo Mmoja