Chama cha soka nchini England, FA, hakitomfungulia mashataka mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa kufuatia kadi nyekundu aliyoonyeshwa wakati wa mchezo wa hatua ya robo fainali wa kombe la FA mwishoni mwa juma lililopita.

FA walitarajiwa kumfungulia mashtaka mshambuliaji huyo, kufuatia picha za televisheni kuonyesha akimfanyia utukutu kiungo wa Everton, Gareth Barry kwa kutaka kumng’ata sehemu za shingoni.

Costa appeared to bite Everton midfielder Barry at Goodison Park during the 2-0 FA Cup quarter-final defeat

Awali ilidhaniwa mshambuliaji huyo kutoka nchini Hispania, alimng’ata Barry, lakini marejeo ya picha za televisheni zilionyesha ukaribu wa tukio hilo na kubainika hakufanya kosa la kung’ata.

Kwa mantiki hiyo sasa Costa, atalazimika kukosa mchezo mmoja ambao upo chini ya chama cha soka nchini England, FA, kutokana na adhabu ya kadi nyekundu iliyomkuta ambayo iliambatana na kadi mbili za njano.

Endapo Costa angebainika alifanya makossa ya kung’ata, angefunguliwa mashataka na angekua katika hatari ya kufungiwa zaidi ya michezo mitatu.

Everton striker Romelu Lukaku scored both of his side's goals in the 2-0 victory over Chelsea on Saturday

Katika mchezo huo, Everton walifanikiwa kusonga mbele kwa ushindi wa mabao mawili kwa sifuri yaliyofungwa na mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji, Romelo Lukaku.

 

Arsenal Wamfuatilia Umar Sadiq
Zlatan Atangaza Msimamo Mkali Wa Kubaki Jijini Paris