Meneja wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta ameikosoa adhabu ya kuoneshwa kadi nyekundu kwa David Luiz kwa kadi nyekundu, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya England Wolves, uliochezwa usiku wa kuamkia leo.

Kwenye mchezo huo Arsenal waliokua ugenini walipoteza kwa kufungwa mabao mawili kwa moja.

Arsenal walikuwa mbele kwa bao 1-0 likifungwa na Nicolas Pepe wakati Luiz akitolewa kwa kadi nyekundu kwa kumchezea faulo Willian Jose – Ruben Neves alifunga Penati iliyosababishwa na Luiz na Wolves walishinda mchezo kwa mabao 2-1.

Arteta amesema kadi aliooneshwa Luiz haikuwa sahihi, na wanajipanga kukata rufaa kupinga maamuzi hayo, ambayo yalipelekea kupigwa mkwaju wa penati.

“Nimeiona mara 10 kwa pembe tofauti na siwezi kukuambia ni wapi kilikuwa na mgusano,” alisema Arteta.

Kwa kadi hiyo, Luiz anatarajia kukosa mchezo ujao wa Ligi Kuu dhgidi ya Aston Villa siku ya Jumamosi, lakini Arteta aliulizwa ikiwa atakata rufaa kwa kadi nyekundu Arteta akasema: “Ninasema ndio, twende moja kwa moja, lakini tunapaswa kuzungumza na kufanya uamuzi kuhusu ni jambo gani bora kufanya.”

“Ikiwa wana pembe nyingine 50 za kuiangalia, labda nitashangaa. Niliangalia pembe saba tofauti na sikuweza kuona migusano yoyote pale”.

Nugaz: Tulieni tutatoa ufafanuzi kuhusu FIFA
Waziri Jafo atoa agizo kwa Afisa Elimu Tabora