Serikali na Jeshi la Polisi nchini, wameshauriwa kuwalinda askari wa usalama barabarani wanaosimamia sheria za uendeshaji wa vyombo vya moto.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa wenyeviti wa kamati za usalama barabarani nchini, Idd Azzan wakati wa kufunga maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani Kitaifa Mkoani Mwanza.

Amesema, askari wa usalama barabarani wanafanya kazi kubwa kudhibiti ajali, hivyo wanapaswa kulindwa na mamlaka zinazowasimamia.

Aidha, amempongeza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini kwa namna alivyochukua hatua dhidi ya kitendo alichofanyiwa askari wa usalama barabarani wakati akitimiza majukumu yake mkoani Dar es Salaam.

Azzan pia ametoa wito kwa wanachi, kuendelea kuheshimu sheria za barabarani ili kupunguza ajali zinazoweza kuepukika na hivyo kupunguza athari zitokanazo na ajali za mara kwa mara.

Ligi ya Tanzania inazidi kupaa Afrika, Duniani
Ibada maalum kumuombea Hayati Dkt. Magufuli yafanyika Chato