Meneja wa klabu ya Sunderland, David Moyes ametozwa faini ya Pauni elfu nane (8,000) pamoja na kufungiwa mchezo mmoja, baada ya kukutwa na hatia ya kutoa maneno makali dhidi ya mwamuzi msaidizi wa mchezo wa kombe la ligi (EFL CUP) dhidi ya Southampton.

Moyes alikishuhudia kikosi chake kikipoteza mchezo wa mzunguuko wa tano wa michuano hiyo kwa kufungwa bao moja kwa sifuri katikati ya juma lililopita.

Katika mchezo huo mwamuzi alimuamuru Moyes aondoke katika benchi la ufundi, kufuatia kauli chafu alizozitoa dhidi ya mwamuzi msaidizi, ambapo alikuwa akilalamikia kikosi chake kuminywa kwa makusudi, hasa baada ya mshambuliaji Victor Anichebe kuangushwa katika eneo la hatari na beki Southampton Maya Yoshida.

“David Moyes atalazmika kukaa mbali na benchi la ufundi la Sunderland, kufuatia kauli zisizo za kiungwana alizozitoa dhidi ya mwamuzi msaidizi,” Imeeleza taarifa iliyotolewa na FA.

“Tukio hilo lilitokea katika dakika ya 90 wakati wa mchezo wa kombe la ligi ambao ulichezwa Oktoba 26 – 2016.

Moyes, mwenye umri wa miaka 53, bado anakabiliwa na mtihani wa kukiongoza kikosi chake katika michezo ya ligi ya nchini England, kwani mpaka sasa hajabatika kupata ushindi tangu alipotangazwa kuwa meneja wa Sunderland.

Alexis Sanchez Afuata Nyayo Za Messi, Mascherano
Klose Astaafu Soka Kwa Heshima, Kuagwa Mwezi Huu