Balozi Ali Karume amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Unguja, Balozi Karume amesema kuwa endapo atateuliwa kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Urais na baadaye kushinda kiti cha Urais wa Zanzibar ataendeleza mazuri yote yaliyofanywa na watangulizi wake.

Zoezi hilo litakamilika Juni 30, 2020 ambapo kwa upande wa Bara fomu zinatolewa katika ofisi za CCM Makao Makuu, Dodoma na kwa upande wa Zanzibar fomu hizo zinatolewa katika Ofisi Kuu za CCM Kisiwandui.

Serikali yapiga marufuku Mgonjwa kudaiwa damu kabla ya huduma

Balozi Karume kwa sasa ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, pia amewahi kuwa Balozi wa Tanzania katika nchini mbalimbali duniani.

Polisi aliyemuua Mmarekani mweusi kwa risasi kushtakiwa

Ngariba maarufu akamatwa Mara

Bungeni: Bajeti ya Serikali 2020/21 yapita kwa kishindo
Majaliwa: vijana msifuate mabinti, miaka 30 itawasubiri