Barabara ya chini ya ardhi inayotumika kusafirisha mihadarati kutoka Mexico hadi Marekani imegunduliwa katika Jimbo la Arizona.

Barabara hiyo iliyokuwa ikitumika kwa siri na wahalifu imegunduliwa na mamlaka nchini Marekani baada ya kufanya uchunguzi wa muda mrefu.

Aidha, Mamlaka nchini Marekani iliigundua barabara hiyo kwenye nyumba moja iliyoko maeneo ya San Luis ambayo inapitia chini ya mpaka hadi kwenye nyumba moja iliyoko San Luis Rio Colorado.

Hata hivyo, barabara hiyo ina urefu wa mita 180 imegundulika mara baada ya mtuhumiwa anayefahamika kwa jina la Ivan Lopez kuwaelekeza polisi kuhusu barabara hiyo.

Congo DRC yawakataa wasimamizi wa uchaguzi wa Kimataifa
NACTE yatoa ufafanuzi ucheleweshaji wa namba ya uhakiki AVN