Nguli wa soka, David Beckham ambaye hivi karibuni alikuwa nchini Tanzania, amezua mjadala wa kimalezi baada ya kuweka mtandaoni picha inayomuonesha akimpa busu zito la mdomo mwanae wa kike.

Baadhi ya wazazi walielezea picha hiyo kuwa haikuwa na maadili na inashangaza kwa kuzingatia kuwa mwanae Harper ana umri wa miaka mitano tu.

“Kwa kuwa mkweli, kumbusu mwanao wa kike mdomoni kama hivi kidogo inashangaza… ndio inashangaza,” aliandika mtu mmoja.

“Ninajaribu kutohukumu lakini nashindwa, lakini nadhani kidogo inashangaza na sio sawa kuona anambusu mwanae kwenye midomo kwa kuzingatia umri wake,” aliandika mwingine.

Hata hivyo, wazazi wenye mtazamo tofauti walijitokeza kumtetea mwanasoka huyo ambaye ni baba wa watoto wanne.

“Ni picha nzuri ya upendo inayoonesha uhusiano mzuri kati yako (Beckham) na binti yako,” aliandika shabiki mmoja. “Achana na wenye chuki. Ni wapumbavu. Harper sio binti mdogo, ni mtoto mdogo tu na hakuna ubaya kwa hilo,” aliandika mwingine.

Hivi karibuni, Beckham alionekana akiingia Tanzania kwa ajili ya kutembelea mbuga za wanyama, akiwa na familia yake. Ujio huo ulionekana kuwa binafsi na wa kimyakimya.

Chukueni hatua kali dhidi ya wasiowasilisha michango-Samia Suluhu
Majaliwa aitaka Halmashauri ya Kilosa kulipa deni kabla juni haijaisha

Comments

comments