Hata kama una utajiri wa kutupwa, kiwango cha ‘kuchunwa’ au kutumia pesa kumfurahisha barafu wa moyo kinapokithiri hujikuta unaacha kuusikiliza moyo na kuangalia salio lako kwanza.

Bilionea James Packer, ameripotiwa kumtosa mchumba wake, Mariah Carey kutokana na matumizi makubwa ya fedha kwa ajili ya manunuzi ya vitu mbalimbali pamoja na starehe.

Kwa mujibu wa chapisho la Australia la Woman’s Day, bilionea huyo anayemiliki casino alichukua uamuzi huo baada ya kuona pia kuwa hata pesa alizowekeza katika kipindi cha runinga alichoanzisha Mariah Carey cha ’Mariah’s World’ zinaelekea kupotea kutokana na kukosa mafanikio.

“Yamekwisha kabisa,” rafiki wa familia ya Mariah Carey aliliambia chapisho hilo wiki hii.

Ingawa wawili hao wameachana, Mariah mwenye umri wa miaka 46 ana mtaji wa pete ya uchumba aliyovishwa na bilionea huyo ya dola za Kimarekani Milioni 10

Kigogo wa polisi, afisa wake watumbuliwa kwa kukutwa na magari ya wizi
Makala: Ali Kiba ajifunze haya kwa Diamond na Diamond afuate haya kwa Kiba