Mkuu wa Chuo Kikuu kishiriki  cha kikristo cha Tiba Kilimanjaro, Profesa Egbert Kessi amesema kuwa wanadai  zaidi ya shilingi  bilioni 1.7 kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB),hali inayopelekea chuo hicho kushindwa kujiendesha.

Profesa Kessi alisema  Bodi kuchelewa kulipa  fedha hizo, kumekuwa kukiathiri uendeshaji wa  chuo kwa kukosa fedha za kulipa waalimu na uendeshaji “Sehemu ya mkopo ambayo inatakiwa kutolewa kwa chuo ndiyo inayochelewa na kusababisha kuwa na deni kubwa zaidi ya sh 1.7 bilioni hivyo kushindwa kuendesha mipango yake kama inavyotakiwa”alisema Prof. Kessi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo Abdul-razaq Badru, alisema kumekuwepo na changamoto ya kulipa fedha kwa vyuo na kwamba malipo yanalipwa kwa utaratibu, ambapo aliongeza kuwa changamoto kubwa inayoikabili Bodi ni wadaiwa sugu kutolipa ili wanufaike na wengine.

 

Jose Mourinho Apata Pigo Old Trafford
Makonda kusafisha uwanja wa fisi