Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ndege la ‘United Airlines’, Oscar Munoz ameuangukia umma akiomba radhi kwa tukio baya lililotokea jana ndani ya ndege ya shirika hilo, ambapo abiria mmoja alitolewa kwa nguvu huku akiburuzwa.

Katika tukio hilo, askari walionekana wakimburuza abiria huyo waliyemchagua kupisha nafasi ya mfanyakazi mmoja wa ndege hiyo baada ya kuonekana kuwa wafanyakazi wote wasingepata nafasi. Hata hivyo, abiria huyo alikataa kutolewa akidai anataka kwenda nyumbani kama ilivyo kwa wasafiri wengine. Alionekana akitokwa damu kutokana na kuburuzwa.

Bosi wa ndege hiyo ameeleza kupitia tamko lake kuwa tukio hilo ni baya na limezisumbua hisia zake. “Hakuna mtu anayepaswa kutendwa visivyo kiasi hicho,” alisema.

Shirika la habari la Associated Press limeripoti kuwa abiria aliyeondolewa kwa kuburuzwa kutoka kwenye ndege hiyo ni mkaazi wa Kentucky mwenye umri wa miaka 65, na kwamba alikuwa na rekodi ya makosa kadhaa ya jinai. Hata hivyo, rekodi hiyo haiwezi kuwa chanzo cha kufanyiwa vitendo visivyofaa kama msafiri aliyetegemea huduma nzuri.

Makundi mbalimbali ya haki za binadamu na huduma za anga yamelaani vikali kitendo hicho cha ndege hiyo inayojinasbu kwa kauli mbiu ya kuwa ‘rafiki safarini’.

Video: Mtikisiko Bungeni, Dk. Mwakyembe azua maswali kuhudhuria mkutano wa Roma
Magazeti ya Tanzania leo Aprili 12, 2017