Brazil imejiondoa kwenye mbio za kuwania uenyeji wa fainali za Kombe la Dunia kwa wanawake mwaka 2023 na badala yake itaiunga mkono Colombia kuandaa michuano hiyo.

Shirikisho la Soka nchini Brazil CBF limesema serikali ya nchi hiyo haioni kuwa ni busara kutoa fedha za maandalizi ya michuano hiyo wakati taifa likiwa katikati ya janga la Virusi vya Corona.

Hadi sasa nchini Brazil kumeripotiwa vifo zaidi ya 35,000 vya Corona huku watu zaidi ya 640,000 wakiwa wameambukizwa ugonjwa huo.

Nchi nyingine zilizosalia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania uenyeji wa fainali za kombe la dunia kwa wanawake mwaka 2023 ni Japan na Australia kwa kushirkiana na New Zealand.

FIFA wanatarajia kumtangaza mwenyeji wa fainali hizo Juni 25 mwaka huu huku fainali hizo zikipangwa kuanza kuunguruma 10 Julai 10 hadi Agosti 20 mwaka 2023.

Mchaka mchaka wa kuwania nafasi za kuwania ushiriki wa fainali hizo umepangwa kuanza mwanzoni mwa mwaka 2021 na kumalizika mwishoni mwa mwaka 2022.

Fainali hizo hushirikisha mataifa 32 kutoka pand zote za dunia, na bingwa mtetezi kwa sasa ni Marekani.

Simu ya Magufuli Mbeya: Tanroad walipeni wananchi
Mchungaji Mashimo ahusishwa uvamizi wa Mbowe