Mahakama kuu kanda ya Iringa imetoa hukumu ya kifungo cha miaka 15 jela kwa Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia ‘FFU’ Pacificius Simon aliye muua bila kukusudia aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa kituo cha Luninga cha channel Ten, Daud Mwangosi.
Hukumu hiyo imetolewa baada ya Mahakama hiyo kumkuta na hatia askari huyo ya mauaji ya bila kukusudia ya Mwangosi yaliyofanyika September 2 – 2012 kwenye kijiji cha Nyololo, Mufindi wakatia CHADEMA ikifanya uzinduzi wa matawi, huku kukiwa na katazo la mikutano au makusanyiko ya kisiasa kutokana na seriakali kuongeza muda wa sensa ya watu na makazi.
CHADEMA watangaza Mikutano, Maandamano Nchi Nzima
PPRA kuzinyoosha taasisi 361 kwa kutowasilisha Mipango yao ya manunuzi (GPN)