Bunge la Seneti la Marekani limepiga kura ambapo katika hali isiyotarajiwa maseneta wa chama cha Republican cha Rais Donald Trump wameonekana kuwaunga mkono wenzao wa chama cha Democratic katika kuishinda kura ya turufu ya Rais, kwa mara ya kwanza katika uongozi wake.

Maseneta hao wameupitisha mswada wa sera ya ulinzi ambao Rais wa Marekani Donald Trump alikuwa ameupinga, ikiwa ni wiki chache kabla kuondoka kwake madarakani.

Walipokutana katika kikao cha nadra katika siku ya maadhimisho ya mwaka mpya, maseneta 81 dhidi ya 13 wamepiga kura na kupata thuluthi mbili inayohitajika ili kuishinda kura hiyo ya turufu.

Kura nane za turufu za Trump zilizopita ziliungwa mkono na seneti.

Wabunge wa republican pia wamepinga shinikizo la wabunge wa Democratic kuongeza malipo ya misaada kwa Wamarekani kwa ajili ya virusi vya Corona kutoka dola 600 hadi dola 2000, nyongeza ambayo Rais Trump anaiunga mkono.

Kwa mujibu wa Sheria za Marekani, Kura ya Turufu ya Rais ya kupinga Muswada inaweza kushindwa iwapo Muswada huo unaungwa mkono na theluthi tatu ya Wabunge katika Mabunge yote ya Congress

DRC: Rais Tshisekedi awasamehe waliofungwa kwa kumuua Kabila
Nchi za Afrika zazindua eneo la biashara huria