Hatimaye Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetaja tarehe rasmi iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wengi ya kumkabidhi uenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli, baada ya mengi kuzungumzwa.

Kamati Kuu ya chama hicho iliyokutana leo katika ukumbi wa Ofisi ndogo ya chama hicho iliyoko jijini Dar es Salam, ikiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Dk. Jakaya Kikwete imeamua kuwa Rais Magufuli atakabidhiwa uenyekiti wa CCM Julai 23 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa ya kikao hicho iliyotolewa leo na msemaji wa chama hicho, Christopher Ole Sendeka, tukio hilo la makabidhiano ya madaraka litafanyika siku hiyo tajwa katika Mkutano Mkuu Maalum.

Ole Sendeka amesema kuwa Mkutano huo Mkuu Maalum utatanguliwa na vikao vya Sekretarieti, Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa.

Lowassa asimulia kisa cha TB Joshua kutohudhuria Kuapishwa kwa Rais Magufuli
Wasiovaa Helmet kwenye Bodaboda kushtakiwa kwa 'kutaka kujiua'