Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemshauri Rais Magufuli kuchukua ushauri kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ili aweze kumshauri kuhusu tatizo la uhaba wa sukari na mfumuko wa bei ya bidhaa hiyo nchini.

Akiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika hivi karibuni Wilayani Monduli, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salim Mwalim ameeleza kuwa suala la sukari hivi sasa limeonekana kushindikana na kwamba mtu pekee anayeweza kumsaidia Rais Magufuli katika hilo ni Lowassa.

“Tatizo la sukari kalianzisha yeye mwenyewe Magufuli na sasa anashindwa kulitatua,” alisema Mwalimu na kuongeza,” Salim Mwalmu alisema. “Mtu pekee atakayemsaidia ni Lowassa. Huyu alijipanga na alijiandaa kuongoza nchi,” aliongeza.

Katika hatua nyingine, Lowassa ambaye alizungumza katika mkutano huo, alisema kuwa amepanga kuanza ziara maalum ya kukijenga chama chao ili kijiimarishe kama chama cha siasa na sio chama cha uanaharakati.

“Nina hakika tumewashika pabaya CCM na tumewaumiza sana. Sasa kwa kushirikiana na viongozi wenzangu tutazunguka nchi nzima tunataka kuiweka Chadema kwenye chama cha siasa na si uanaharakati,” alisema Lowassa.

Mwanasiasa huyo mkongwe ambaye aligombea nafasi ya urais mwaka jana kupitia Chadema akiungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa alisema anaamini siku moja atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Makonda azilima Benki zilizopokea mishahara ya watumishi hewa
Familia ya Marehemu Kabwe yakananusha kutoishirikisha Serikali Mazishi