Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kimesema muendelezo wa kukamatwa kwa viongozi wa chama hicho hakuwayumbishi bali kunawajenga kisiasa.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Vicent Mashinji alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  na kueleza kuwa suala hilo halitachukua muda mrefu kwenye utekelezaji.
“Hapa tunapoongea Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime, Misiwa ameshikiliwa na jeshi la polisi,Tundu Lissu yuko mikononi mwa polisi na Mbowe anahitajika,” amesema Dkt. Mashinji.
Amesema Watanzania wanapaswa kukemea suala hilo kwa kupaza sauti zao zifike mataifa mbalimbali wafahamu ukiukwaji wa sheria unavyoendelea.
Aidha, kwa upande wa Jeshi la polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam kupitia kwa Kamishna Simon Sirro, amesema wataendelea kumhoji Tundu Lissu mpaka mpaka watakapo maliza upelelezi wao pamoja na uchunguzi, hivyo inaweza kuchukua zaidi ya siku nne.

Video: Makonda ataja mtandao mpana dawa za kulevya, Maskini wema...
Tundu Lissu agoma kula, adai mpaka afikishwe mahakamani