Nyumba ya mama Wema Sepetu, Mariam Sepetu, iliyopo Sinza Mori jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia jana imepigwa mawe juu ya bati kwa muda wa saa moja na nusu, kutokana na tukio hilo viongozi wa Chadema wamechukua hatua ya kuweka ulinzi mkali nyumbani hapo na kuzungumza kuwa wamegundua kitu ambacho hawatakiweka wazi kwa sasa.

Baada ya tukio hilo kutokea mama Sepetu aliwasiliana na mwanae Wema Sepetu pamoja na viongozi wa Chadema, ambapo Meya wa Ubungo, Boniface Jacob alifika na kuangalia hali ya mama huyo na kuamua kuweka ulinzi.

”Tumeshaangalia mazingira yote tumegundua kitu ambacho hatuta kiweka wazi kwa sasa ila tutaweka ulinzi mkali na atakaye jaribu shauri yake hatuta kubali suala hili liendelee kumkuta kamanda wetu na mimi mara kwa mara nitafika kuangalia mazingira” amezungumza hayo Meya wa Ubungo, Boniface Jacob.

Meya alifafanua kuwa ulinzi huo hautaishia nyumbani kwa mama Wema bali hata nyumbani kwa Wema Sepetu ulinzi utaimarishwa kwani amegunf=dua wanachama hao wapya wamekuwa wakiwindwa na watu wasiojulikana.

Wema alipohojiwa amesema, ” Mama yangu ameteseka usiku kucha kwa kukosa amani, amelia na kukosa hata hamu ya kula tumefika tumemkuta katika hali mbaya, najua yana mwisho ila tutazidi kufanya dua ya kumwomba Mungu atuepushie na mabaya yote,”.

Mama nae alihojiwa na kusema, ” sikuweza kutoka nje kwa kuwa najua mbaya wangu amekaa wapi na amekusudia kufanya nini,”.

Video: Wananchi 214 Dar kupewa hati
Video: Lukuvi amtikisa Makonda, Jaji amshukia mwendesha mashtaka kesi ya Lema