Serikali za China na India, zimetoa wito wa kufikiwa kwa makubaliano ya kumaliza vita nchini Ukraine hatua, inayoashiria kwamba washirika hao wa Urusi sasa wanaonyesha kuigeuzia mgongo sera ya uvamizi.

Nchi hizo, zimetoa wito wito huo kwenye mkutano wa kilele wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, mjini New York nchini Marekani na hakukuwa na taifa lolote kubwa lililoiunga mkono Urusi, hata China ambayo siku chache kabla ya Urusi kuivamia Ukraine mwishoni mwa mwezi Februari iliapa kuimarisha mahusiano yake na rais Vladimir Putin.

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi ametoa wito kwa Urusi na Ukraine kujizuia ili kuepusha mzozo huo kusambaa zaidi, lakini pia kutoathiri zaidi mataifa yanayoendelea na kusema, “China inarunga mkono juhudi zozote za azimio la amani katika mzozo wa Ukraine. Kipaumbele cha msingi ni kuandaa mazungumzo ya amani.”

China na India wametoa mwito huo kwenye mkutano wa kilele wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, mjini New York. Picha na AP.

Puttin apata ‘kigugumizi’ usaidizi wa china kwa Urusi

Wakati wa ziara yake kwenye Umoja wa Mataifa, Wang alikutana na waziri wa mambo ya nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba, katika mazungumzo yao ya kwanza tangu vita hivyo vilipoanza. Mapema mwezi huu.

India, tofauti na China ina mahusiano mazuri na Marekani lakini pia ina mahusiano ya kihistoria na Urusi, ambayo imekuwa msambazaji wake wa silaha kwa muda mrefu. “Wakati mzozo wa Ukraine ukiendelea kufukuta, mara nyingi huwa tunaulizwa msimamo wetu,” alisema waziri wa mambo ya nje wa India Subrahmanyam Jaishankar.

“Jibu letu, kila wakati ni la moja kwa mola na la kweli–India iko upande wa amani na itaendelea kusimamia hilo kwa uthabiti,” alisema. “Tuko upande unaotaka mazungumzo na diplomasia kama njia muafaka ya kumaliza mzozo huo.”

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov anayashutumu mataifa ya magharibi kwa kutaka ulimwengu kuichukia Urusi

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov kwenye mkutano na waandishi wa habari alikataa kujibu swali la iwapo kumekuwepo na shinikizo kutoka kwa China. Kwenye hotuba yake, alitaka kuyamwagia lawama mataifa ya magharibi.

TPA yatoa tamko ujenzi Bandari ya Bagamoyo
Wanachama ACT wahimizwa uwajibikaji