Klabu ya Schalke 04 ya nchini Ujerumani, imethibitisha kumsajili beki wa kulia kutoka nchini Hispania Jorge Andújar Moreno “Coke”, akitokea Sevilla CF.

Taarifa ya uthibitisho iliyotolewa na klabu ya Schalke, imeeleza kuwa, usajili wa beki huyo mwenye umri wa miaka 29, umewagharimu kiasi cha Euro milion 5.

Coke anaondoka nchini Hispania huku akikumbukwa alijiunga na Sevilla CF mwaka 2011 akitokea Rayo Vallecano, na alifanikiwa kuwa nahodha wa mabingwa hao wa Europa League mara tatu mfululizo.

Claudio Ranieri: Nimechoshwa Na Taarifa Za Riyad Mahrez
Happi Awapa Wasanii Mikakati ya Kujikwamua na Umaskini