Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, ameweka wazi mipango yake ya kutaka kucheza soka kwa miaka kumi ijayo, akiwa katika kiwango chenye ubora kama ilivyo sasa.

Ronaldo aliweka wazi mipango hiyo, saa chache baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano wa kuendelea kuitumikia Real Madrid jana mchana, ambapo kitendo hicho kilishuhudiwa na waandishi wa habari pamoja na familia yake.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31, amesaini mkataba huo ambao utamuwezesha kulipwa mshahara wa Pauni laki tano (500,000) kwa juma.

Image result for Cristiano Ronaldo hopes for 'another 10 years' after signing new deal at Real MadridCristiano Ronaldo akiwa na familia yake pamoja na watu wa karibu, kulia kwake ni rais wa Real Madrid Florentino Perez na kushoto kwake ni mama yake mzazi.

Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano, Ronaldo alisema amepanga kucheza soka kwa kipindi cha miaka kumi ijayo na anaamini atakuwa katika kiwango cha ubora.

Alisema dhamira hiyo amekua nayo kwa muda mrefu, na jana ilikua ni siku maalum kuiweka hadharani kufuatia furaha iliyokua imekithiri moyoni mwake, kutokana na hatua ya kusaini mkataba mpya ambao utaendelea kumuweka Santiago Bernabeu hadi mwaka 2021.

“Bado nina muda mrefu wa kucheza soka, naamini nitakua uwanjani kwa kipindi kingine cha miaka kumi ijayo, na ninataka kuendelea kuwa katika kiwango changu.” Alisema Ronaldo.

Ronaldo, alijiunga na Real Madrid mwaka 2009 akitokea Man Utd, na tayari ameshavunja rekodi ya aliyekua mshambuliaji wa The Meringues Raúl González Blanco aliyefunga mabao 360, lakini kwa nahodha huyo wa Ureno ameshafikisha mabao 371.

Maneno matatu ya mwisho ya Sitta yawekwa wazi, ni funzo zito
Ratiba Ya Mzunguuko Wa Pili FA CUP 2016/17