Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) ambaye pia alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, ameondolewa ulinzi wa serikali aliokuwa nao na kubaki na mlinzi mmoja pekee.

Taarifa zilizothibishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF, Hamad Masoud zimeeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imemuondolea ulinzi huo tangu siku aliyoapishwa Rais Ali Mohamed Shein.

Maalim Seif alionekana kwa mara ya kwanza akiwasili katika ofisi yake ya chama iliyoko Vuga akiwa na gari la Serikali pamoja na mlinzi mmoja pekee, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo alikuwa akisindikizwa na Polisi pamoja na ving’ora.

Akizungumzia suala hilo, Masoud alisema kuwa hatau hiyo ya serikali imechukuliwa kama adhabu kwa Maalim Seif kutokana na uamuzi wa chama hicho kususia uchaguzi wa marudio.

Hata hivo, aliwataka wafuasi wa chama hicho kutokuwa na wasiwasi na usalama wa mwanasiasa huyo kwakuwa anapewa ulinzi wa kutosha na kitengo cha ulinzi cha chama hicho.

Julio Aisikitikia Simba Iliyoshindwa Kuifunga Coastal Union
Viporo VYa Ligi Kuu Kuendelea Kesho