Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Victoria Mwanziva ameipongeza Mahakama ya Wilaya ya Ludewa kwa kutoa elimu ya Sheria kwa wananchi na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii wakati wa kilele cha wiki ya sheria nchini.

Mwanziva ambaye alikuwa ni mgeni rasmi, ameyasema hayo katika Maadhimisho ya kilele cha siku ya Sheria Nchini, ambayo kiwilaya yalifanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe.

Kwa upande wake, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ludewa, Isaac Ayeng’o wakati akitoa Taarifa ya mafanikio ya matumizi ya TEHAMA katika shughuli za kimahakama amesema kuwa “Mahakama kupitia mtandao yake inawawezesha wateja wa mahakama wenye KOMPUTA, VISHIKWAMBI PAMOJA NA SIMU JANJA kuweza kupata taarifa mbalimbai za mahakama”.

Amesema, kwasasa Mahakama inatoa huduma kwa njia ya TEHAMA ili kuongeza uwazi,kupunguza gharama wakati wa ufunguaji mashauri, kupata taarifa za mashauri, kufanya malipo ya ada za mashauri lakini pia mahakama imefanikiwa kusikiliza hukumu mbili kwa njia ya video.

Serikali yalaani Wananchi kuvamia, kuuwa Askari
Milango ipo wazi uwekezaji sekta ya Nishati: Makamba