Chama cha Democratic nchini Marekani kimemtaka Rais wa nchi hiyo Donald Trump kutoingilia uchunguzi unaofanyika dhidi ya tuhuma zinazomkabili za kushirikiana na Urusi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

Trump anatuhumiwa kushirikiana na Urusi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kudukua nyaraka mbalimbali za aliyekuwa mpinzani wake kutoka chama cha Democratic nchini humo, Hilal Clinton.

Aidha, kiongozi mkuu wa chama cha Democratic, Nancy Pelosi amesema kuwa kama Rais Trump ataruhusu uchunguzi ufanyike kwa uhuru basi kila mmoja atakua hana mashaka naye hata ndani ya chama chake.

Mkuu wa Upelelezi wa zamani wa FBI, Robert Mueller ameteuliwa kuongoza jopo la uchunguzi huo lakini bado kuna wasi wasi mkubwa kwa Democratic na watu mbalimbali kuwa jopo hilo halitatoa taarifa sahihi sababu bado litakuwa chini ya uangalizi wa Rais Donald Trump.

Hata hivyo, kwa upande wake Trump amesema kuwa ameingia katika vita kubwa katika historia ya sisa nchini Marekani kitu ambacho hakukitarajia katika maisha yake.

Video: Hali mbaya Kibiti, Meya Arusha, viongozi wa dini mbaroni kwa amri ya Gambo
Magazeti ya Tanzania leo Mei 19, 2017